UJERUMANI YAIBUKA BINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2014 DHIDI YA ARGENTINA.
Hatimaye fainali za kombe la dunia zilizo anza rasmi tarehe 12/06/2014 kule nchini Brazil zimefikia tamati usiku huu, huku timu ya Ujerumani ikiibuka mshindi wa kombe la dunia 2014 baada ya kuifunga timu ya Argentina goli 1-0 katika dakika za nyongeza, mnamo dakika ya 110.
Mtanange huu wa fainali uliokuwa mkali huku timu zote zikishambuliana kwa zamu, hatimaye timu ya Taifa ya Ujerumani imeweza kuibuka kidedea baada ya mchezaji Mario Gotze wa Ujerumani kuifungia timu yake ya Taifa goli pekee na kuiwezesha Ujerumani kuwa mabingwa wapya wa kombe hili dhidi ya wapinzani wao Argentina, mechi hii imechezwa katika dimba la Maracana jijini Rio de Janeiro.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani

Mario Gotzeakitupia goli pekee la ushindi.

Goal! Mario Gotze akiipatia Ujerumani goli la ushindi.
Comments
Post a Comment