KAMA NI MDADA SOMA HAPA PANA KUHUSU

Ujumbe huu nimeukuta whatsapp katika group ambalo marafiki tunalitumia katika kubadilishana mawazo, sasa kama wewe ni mdada chukua japo dakika mbili kusoma ujumbe huu.

"Huwa napata shida sana nikikutana na Wasichana
wenye hii tabia...Unampenda
Msichana kabisa kutoka moyoni unajipanga unamtongoza...anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,'' Oh my Ghosh, ur still a kid, mi nadate
guys who are 45 years above. Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana
mnasumbua sana''.

Sio tunasumbua, anajua kabisa
miaka 29 bado ndo unasaka hela, ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi! Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47...Uongo mtupu! Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45?  Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga, amefanya kazi ana hela, unajifanya unampenda
kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni, hamna hata
aibu.

Mnapenda sana vitu ready made, tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha
hapo alipo, we unakuja unadandia tu, Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani, msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti he's caring uone inavyouma, utatamani
umpige patasi ya kisogo......Gold diggers, waone kwanza, msione gesi mtwara mshaanza kuandamana! 45 years guy waiting for u student of 23 years, ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??"

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA