Mchungaji Christopher Mtikila aenda kortini kuomba aingzwe kwenye kesi ya IPTL vs Kafulila
Awali, Kafulila akizungumza kwenye mjadala katika eneo la Urusi Mwanga
mjini Kigoma jana, alisema Mchungaji Mtikila ameomba kuwa mshitakiwa wa
pili katika kesi hiyo huku Chama chake cha DP kikiwa mshitakiwa wa tatu.
Pia alisisitiza kuwa kamwe hakukurupuka kuibua kashfa hiyo ya ufisadi katika akaunti ya Escrow na
kwamba, yuko tayari kwa lolote.
“Nimefarijika kuona wenzangu wananiunga mkono katika mapambano dhidi ya ufisadi na Mchungaji Mtikila ameomba kuwa mshitakiwa wa pili,”
alisema Kafulila.
Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila, alikiri kuwa amekubali kuunganishwa kwenye kesi hiyo inayomkabili Kafulila.
Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila, alikiri kuwa amekubali kuunganishwa kwenye kesi hiyo inayomkabili Kafulila.
“Nimekubali kuunganishwa katika kesi hiyo ili kutetea haki ya wananchi wa nchi yetu kama Katiba inavyosema,”
alisema.
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), imefungua
kesi ya madai dhidi ya Kafulila katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es
Salaam, ikiomba aamriwe kuilipa fidia ya sh. bilioni 310 kutokana na
kutangaza taarifa za kashfa dhidi yao na hasara ya taswira ya biashara
na hadhi yao.
Fadhili Abdallah, Kigoma
safi sana mchungaji najua we mpambanaji mtashinda
ReplyDelete