ALIKIBA AFUNGUKA LIVE KUHUSU CHANZO CHA BEEF KATI YAKE NA DIAMOND MWANZO MWISHO.


Alikiba aweka wazi chanzo cha beef kati yake na Diamond, akiri yeye ni shabiki wa nyimbo za Diamond
Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa bongo fleva wiki hii ni pamoja na kusikia kauli ya Alikiba kuhusu chanzo cha beef kati yake na msanii mwenzake Diamond Platnumz.
Kupitia kipindi cha Sporah kilichoruka July 22 Clouds TV, Alikiba amefunguka mambo mengi ikiwemo jinsi walivyofahamiana kwa mara ya kwanza, chanzo cha beef yao na wakoje hivi sasa.
Kabla hujafahamu undani wa alichokizungumza, hizi ni facts chache alizozitoa Alikiba katika Interview hiyo.

1.Alikiba ndiye alimpa ruhusa Bob Junior amrekodie Diamond nyimbo zilizomtoa kama ‘Kamwambie’ katika studio yao ya Sharobaro!

2.Alikiba alishirikishwa katika wimbo wa Diamond ‘Lala Salama’!

3. Alikiba ni shabiki wa nyimbo za Diamond hadi sasa!

4. Diamond aliomba ashirikishwe katika hit ya Alikiba ‘Single Boy’!

5. Alikiba ana watoto watatu, lakini hana uhusiano tena na mama zao
Asilimia kubwa ya kipindi ilihusu uhusiano wa Alikiba na Diamond, na hii ni sehemu ya maelezo ya Kiba.

Alikiba aliizungumzia sababu iliyozaa beef kati yake na Diamond, swali la Sporah lilikuwa kama Alikiba ana namba ya simu ya Diamond:

“Nilikuwa nayo kipindi Fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima…kuna kipindi alinikosea kwasababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ile nyimbo ya ‘Single Boy’, na si kweli. Halafu anasema mimi ndio nilimfuta…
kwa kunikosea kwa Diamond nilihakikisha kutokana na mimi mwenyewe ndo nilifanya nyimbo yake ‘Lala Salama’ iko kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichonituma nifanye nimefanya kwa mapenzi yote, na mimi namsupport kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri anayeimba vizuri, sikatai anaimba vizuri sijui ukisema ame copy am proud, mi sijamaind wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya ukaonekana mi sifai, siko hivyo mimi.”
Aliendelea,

“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Alikiba. wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nimemfuta Diamond kwenye nyimbo ya ‘Single boy’ lakini mimi wala, shahidi producer Manecky ndo alitengeneza ile nyimbo. Sikuwahi kwenda na Diamond kwenye studio na sikuwahi kufikiria kufanya nyimbo nae.

Ila alinipigia simu baada ya ile nyimbo kuleak, imevuja Single boy, tayari nimeshafanya na Jaydee, akaisikia kwenye simu Ali kuna nyimbo nimeisikia unaonaje ile tukifanya ile itakuwa safi sana afu akanipa mpaka idea ya video na nini, nikamwambia sawa inawezekana lakini mimi nadhani itapendeza zaidi tukifanya nyimbo nyingine mimi na wewe,kwasababu hii tukifanya mimi na wewe haita make sense inapendeza ikiwa single boy single girl, hicho ndo kitu nilimjibu.

Akaniambia poa lakini we fikiria hiyo, nikamwambia okay lakini hata kama nikifikiria mi sioni jibu hapo, jibu ni hilo hilo. Hicho ndo kitu ambacho nilimjibu Diamond. Baada ya kama wiki moja nikaja kusikia kwenye mablog, mpaka nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta kwenye ile nyimbo wakati yeye ndio aliyenifuta katika nyimbo yake, shahidi producer wangu mimi KGT anaitwa ambaye nimetoka naye muda mrefu sana..nyimbo zangu zote alikuwa akiproduce yeye”.

Kuhusu nani aliyemuita mwenzake kwaajili ya wimbo ambao Alikiba anadai Diamond alimfuta (Lala Salama)

“Hakuna aliyemuita mwenzake, ila mimi pale studio ambayo alikwenda kurekodi Diamond ni studio ya kwangu mimi ambayo ilikuwa imenitoa pale G-Records na watu wote wanajua nimetokea pale. ..Nakwenda kutembea kama nyumbani , kuwatembelea studio kumtembelea producer wangu, nikamkuta Diamond nae studio anarecord.

Kuingia pale ndani ya studio nikakuta amesha record kabisa…akaniambia hebu sikiliza hii, nikasikiliza nikamwambia umeimba vizuri sana…nikajaribu kumwambia ungeimba hivi na hivi na hivi ingekuwa vizuri sana ila niliheshimu mamuzi yake kwasababu kila mtu na style
chanzo:Bongo5

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA