DUNGA KOCHA MPYA WA TIMU YA BRAZIL


dunga_1a8e0.jpg
Brazil imemtangaza mchezaji wa zamani Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa, kwa mara ya pili. Dunga alikuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994 waliposhinda Kombe la Dunia, na alikuwa kocha kuanzia mwaka 2006 hadi 2011.

"Nimefurahi sana kurudi," amesema Dunga, 50, ambaye alikuwa akitajwa sana kuchukua nafasi hiyo. Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari, aliyejiuzulu baada ya Brazil kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014, lakini alipata kipigo kizito katika historia ya taifa hilo kwa kufungwa 7-1 na Ujerumani. Dunga aliifikisha Brazil katika robo fainali Afrika Kusini mwaka 2010.


MJENGWA.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA