RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa
zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck
Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yamekamilika na kuongeza
kuwa maadhimisho ya mwaka huu kihistoria yanalenga kuwaenzi wote
waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa ardhi ya Tanzania,
kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.
Amesema maadhimisho hayo
yatapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Gwaride la Kumbukumbu
litakaloonyeshwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT). Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na uwekaji na
silaha za asili, maua kwenye mnara wa kumbukumbu pamoja na viongozi wa
madhehebu mbalimbali ya dini kutoa dua na sala kuliombea taifa.
Bw. Sadiki amefafanua kuwa
shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi
na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu
hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea
uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote
muhimu ya uwanja huo. Aidha, katika hatua nyingine ameeleza kuwa wakati
wa maadhimisho hayo barabara ya Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa
kwa muda kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara hizo
watakaohudhuria maadhimisho hayo.
Comments
Post a Comment