ZIMEBAKI SIKU 3 ALIKIBA KUACHIA NGOMA MPYA,JE ATARUDI KWA KISHINDO?


Zikiwa zimebaki siku 3, mkali wa Cindelera na hit song kibao Ally Kiba, anatarajia kudrop single mpya mtaani wiki hii. Msanii huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu na kupelekea  baadhi ya mashabiki wake kuhoji kila mara nini hasa kimemsababisha mkali huyu aliyewahi kukutana katika ngoma moja na msanii R.kelly katika nyimbo iliyokutanisha wasanii mbalimbali kutoka bara la Afrika.inayoitwa "One 8".

Ally Kiba amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na msanii anayefanya vizuri kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, mpaka kupelekea kuwa na marumbano ya mara kwa mara na wakati mwingine kutishiana kabisa. Swali lililopo vichwani mwa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva je Ally Kiba atakuja kwa nyimbo gani kali ambayo itaweza kumkalisha hasimu wake? BASI TUSUBILI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA