JAMES RODRIGUEZ ATAIMUDU ADA YAKE YA UHAMISHO REAL MADRID?

1406055395787_wps_11_Colombian_striker_formerlNa Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao
KULIKUWA na maswali mengi zaidi kuliko majibu kufuatia James Rodriguez kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 80 sawa na paundi milioni 60 kutokea klabu ya Manaco.
Wapi Mkolombia huyo atacheza?  anastahili ada kama hiyo ya uhamisho?, kweli Real Madrid inamhitaji yeye?
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez hana wasiwasi. Kiwango kikubwa alichoonesha katika fainali za kombe la dunia akiwa na taifa lake ndio sababu ya Real kumsajili majira haya ya kiangazi.

Usajili huo umekuwa mkubwa zaidi ya Toni Kroos aliyesaini mkataba wa miaka sita na mabingwa hao wa Ulaya wiki iliyopita.
Licha ya kipaji alichonacho Rodriguez, mashabiki wa Real Madrid wamebaki wakishangaa kama kweli mchezaji huyo mpya atakayevalia jezi namba 10 atang’ara na klabu kama alivyofanya Brazil akiwa na Colombia.

Mchezaji huyo wa zamani wa Porto alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa kombe la dunia kwa kufunga magoli sita na kuiongoza Colombia mpaka hatua ya robo fainali.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA