VURUGU KUBWA YAZUKA ARGENTINA BAADA YA KUFUNGWA FAINALI

Polisi wa Argentina wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu, Buenos Aires baada ya nchi hiyo kufungwa na Ujerumani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia.

Mapema jana jioni maelfu ya watu walikusanyika katika mnara wa Obelisk jijini humo ili kusherekea licha ya kupoteza mchezo huo.
Hata hivyo, baadaye usiku, hali ilibadilika na vijana kuanza kuwarushia polisi mawe na kuvunja maduka. Watu wasiopungua 50 walikamatwa huku polisi 15 wakijeruhiwa





chanzo:Salim Kikeke

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA