LEBRON JAMES AAMUA KURUDI TIMU YAKE YA ZAMANI CLEVELAND

LeBron James katika picha

Mchezaji nyota wa mchezo wa basketball nchini Marekani LeBron James ametangaza kuwa ataondoka timu ya Miami Heat na kurudi timu yake ya zamani Cleveland Cavaliers.

Uamuzi huo wa LeBron James ulikuwa unasubiriwa kwa hamu baada ya Miami Heat kushindwa katika fainali ya ligi na San Antonio Spurs mwanzoni mwa mwezi Juni. LeBron James alishinda ubingwa wa NBA mara tatu na timu ya Miami Heat.

Kabla ya kwenda Miami Heat LeBron James aliichezea Cleveland Cavaliers timu ambayo ilimchukua toka shule ya sekondari, na kuondoka kwake katika timu hiyo miaka minne iliyopita kuliwakasirisha sana wakazi wa Cleveland.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA