REMY CABELLA ATUA NEWCASTLE UNITED
Kijana mpya: Remy Cabella akipozi katika picha ndani ya dimba maarufu la St. James` Park baada ya kukamilisha uhamisho.
Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 9:32 usiku
Newcastle United imekamilisha usajili wa Remy Cabella kwa dau la paundi milioni 12.
Kiungo huyo wa zamani wa Montpellier
alisafiri mpaka Tyneside kukamilisha vipimo vya afya na rasmi amekuwa
mchezaji wa Newcastle.
Cabella amekuwa mchezaji wa kwanza ghali kusainiwa na Magpies tangu alipomnunua Michael Owen mwaka 2005 kwa paundi milioni 16.
Mwanzo mzuri: Cabella (kushoto),
aliyepigwa picha akichuana dhidi ya Bastia msimu uliopita anakuwa
mchezaji wa nne kusajili na Newcastle majira haya ya kiangazi.
Hatua kubwa: Cabella (kulia) alikuwa
sehemu ya kikosi cha Ufaransa katika fainali za kombe la dunia mwaka huu
nchini Brazil, lakini hakucheza mechi yoyote.
Kocha Alan Pardew alijaribu kumsajili
Cabella katika dirisha dogo la usajili la mwezi januari baada ya Yohan
Cabaye kuondoka na kujiunga na Paris St Germain na mwisho wa siku ndoto
yake imetimia.
"Huu ni usajili ambao kiukweli nilikuwa
nahitaji," alisema Cabella. "Sijasikia lolote, zaidi ni mazuri tu kuhusu
Newcastle United kwa kila mtu niliyeongea naye".
"Nilitaka kujiunga na klabu kubwa ya
England na ndio sababu nimefika hapa. Naangalia mbele kufanya kazi kwa
bidii na kucheza kwenye uwanja mkubwa na nitaisaidia klabu hii kwa uwezo
wangu wote".
Kocha wa Newcastle United Alan Pardew
alisema: 'Remy ni mchezaji ambaye amekuwa kwenye rada zetu kwa muda
mrefu na tumefurahi kumleta klabuni".
chanzo:bkmtata
Comments
Post a Comment