PAMBANO DHIDI YA MYWEATHER NA PACQUIANO LAZIDI KUNUKIA


Juzi bondia Floyd Mayweather alijisalimisha mwenyewe jela huko Las Vegas kutumikia kifungo cha siku 87 kutokana na kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani mbele ya watoto wao.

Hata hivyo hatua hiyo haijaathiri pambano linalongojewa kwa hamu kuliko yote kati yake na mfilipino Manny Pacquiao. Habari njema ni kuwa mabondia hao sasa hivi wanazungumza moja kwa moja.

Kwa mujibu wa mwalimu wa Pacquiao Freddie Roach pambano hilo linanukia.

“Golden Boy (promota wa Mayweather) na (Arum, promota wa Pacquiao) wanachukiana kiasi ambacho wameamua kukaa pembeni. Kwahiyo Manny na Floyd wameanza kuongea wenyewe, ” alisema Roach.

“Watagawana 40-40 na mshindi atachukua hela ya ziada. Kitu ambacho ni sawa sababu kila mmoja anasema atashinda.”

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA