HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIPOFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012
Mhe. Phillipo Mulugo (MB)Naibu Waziri wa Elimu akisoma hotuba yake
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Phares Magesa
(Wa
Pili Kulia,Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro(Wa
Kwanza Kushoto)Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks(wa
kwanza Kulia),Brand Manager msaidizi
wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto),Hashim Thabeet(Wa Pili Kushoto)
Baadhi ya Vijana Walioshiriki Clinic Ya Sprite Hasheem Thabeet 2012
---
Mkurugenzi wa Michezo,
Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu Phares
Magesa,Afisa Utamaduni Ubalozi wa Marekani, Danna Banks,Brand Manager
msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro,Hasheem Thabeet ,Viongozi wa
TBF,Makocha,
Wachezaji na wadau wote wa michezo.
Kwa
niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi
hii kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo
haya yanafanyika katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru
Coca cola kupitia kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa
Mpira wa kikapu hasa katika
ngazi
ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi
wao hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia
mchezo wa kikapu.
Kipekee
na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika
mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya
Vijana wadogo kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu ili nao
wapate kuwa na ndoto
na kufika pale alipo yeye
Nimatumaini
yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi
kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu
ambao hawakupata nafasi kama hii mliyoipataMikoa iliyoshiriki kliniki
hii ya mwaka huu ni
Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.
Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.
Ndugu
zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo kama mnavyofahamu wote
kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi
mashuleni, hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia
kuwaimarisha kimbinu za
kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.
kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.
Serikali
itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika
kuhakiksha michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu
wengi zaidi wakasomee taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa
ni sambamba na kuongeza uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu kufundisha
michezo.
Narudia
tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu
kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la
kila mmoja wetu, wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote
nchini kuhakisha vijana wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.
Nafahamu
kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika
nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na
wadau wengine kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika
ngazi zote.
Maombi
yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja
mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha
wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha
katika ngazi husika ili yaweze kushugulikiwa.
Nawashukuru
sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE
naHasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga
mfano wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya
watanzania na nia yake
njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.
njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.
Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani mchezo wa kikapu.
Niwatakie
Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru
wotekuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika
kuchangia kufanikisha
malengo yenu.
malengo yenu.
Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.
Mhe. Phillipo Mulugo (MB)
Naibu Waziri wa Elimu
Comments
Post a Comment