PROFESA MAJI MAREFU ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI DODOMA


Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani), leo amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini.

Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni Dodoma.

Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo  Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda  alilazimika kuingilia kati kumzuia Profesa Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA