MTU MZIMA DAWA KULIPUKA@VILLA PARK MWANZA

  ONYESHO lililopewa jina la Mtu Mzima Dawa ambalo litafanyika Julai 6 (Ijumaa) kwenye Viunga vya Villa Park jijini Mwanza linatarajiwa kuwa bab kubwa.

Akizungumza jana Meneja wa Kundi la TMK Family ambao ndio wandaaji wa onyesho hilo, Said Fella amesema litakuwa onyesho la pekee ambalo halijawahi kutokea Mwanza.

“Onyesho la mtu mzima dawa kwenye Ukumbi wa Villa Park Julai 6, litakuwa bab kubwa sana, yaani itakuwa ni mlipuko,” alisema Fella.

“Tumeandaa wasanii wazuri wenye vyimbo zinazotamba sasa, ambao wamejipanga vyema kwa ajili ya kufanya makamuzi ya kuilipua Villa Park.”

Fella aliwataja wasanii watakaoshiriki kwenye onyesho hilo la usiku wa mtu mzima dawa kuwa ni Bibi Cheka, ambaye ndiye mhusika mkuu wa onyesho hilo.

Wengine watakaomsindikiza ni Chegge, Temba, Aslay kutoka TMK Family, Ommy Dimpoz, Mwana FA na Ferouz. 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA