AZAM YAFANYA KWELI HATIMAYE WATU KWENDA ZANZIBAR KWA MAGARI YAO KUPITIA MELI YAO MPYA NA YA KISASA KABISA

 Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
 Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
---- .
Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni  kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. 

 Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

Comments

  1. kampuni inayojua kutumia fursa, haina siasa wala ubabaishaji! BIG UP! ....JP

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA