JK aisaidia taasisi ya mkapa kuchangiwa shilingi bilioni 3.2 katika harambee
Rais
Jakaya Kikwete akimpongeza Bw Deo Mwanyika, Makamu wa Rais wa Kampuni
ya Barrick Tanzania baada ya Kampuni hiyo kuchangia dola laki 5 za
kimarekani na kuongoza katika harambee ya kuchangia fedha programu ya
Mkapa Fellows inayoendeshwa na Taasisi ya HIV/AIDS ya Mkapa (Benjamin
Mkapa HIV/AIDS Foundation) usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency. Kushoto ni Rais mstaafu, Benjamini Mkapa na
kulia Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi
Rais
Jakaya Kikwete, akimkabidhi Picha ya kuchora Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya UNDI Consulting Group Limited, Injinia Philip Makoka baada
ya kuinunua wakati wa Harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa
Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika Dar es
Salaam kwenye Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency usiku wa kuamkia leo
Rais
Jakaya Kikwete akimkabisdhi moja ya vito Mkurugenzi Mtendaji wa Hotel
ya Kibo Palace ya jijini Arusha Bw. Vincent Laswai baada ya kununua kwa
Sh Milion 12 wakati wa harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa
Fellows inayoendeshwa na Taasisi ya HIV/AIDS ya Mkapa (Benjamin Mkapa
HIV/AIDS Foundation)
Rais
Jakaya Kikwete, akimkabidhi jiwe la Tanzania aliyelinunua kwa dola za
Kimarekani 13,000 wakati wa Harambee ya kuchangia fedha programu ya
Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika
Dar es Salaam kwenye Hotel ya Kempinsik Dar es Salaam juzi usiku. Kulia
ni Balozi Amy Mpungwe ambaye kampuni yake ya Tanzanite One ndio
iliyochangia jiwe hilo
Rais mstaafu, Ali Hassani Mwini akimkabidhi Picha ya marais wanne Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited, Bw William Chiume baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh Milion 13 wakati wa Harambee ya kuchangia Fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa na kwa Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS Foundation. |
Taasisi
ya Mkapa usiku wa kuamkia leo imekusanya shilingi bilioni 3.2 kupitia
harambee ya mchango uliotolewa kwenye chakula cha hisani kwenye hoteli
ya Kempinski, Jijini Dar es Salaam.
Kiwango
hicho cha fedha kimepitiliza lengo lililokusudiwa na taasisi hii ambalo
lilikuwa ni kukusanya shilingi bilioni 3 kupitia program ya Mkapa
Fellows ambayo inalenga kuendesha miradi ya kusaidia huduma za afya
nchini hasa maeneo ambayo huduma hizo ni hafifu. Huduma hizo zimejikita
zaidi katika maeneo matatu; kuimarisha huduma kwa waathirika wa Virusi
Vya Ukimwi (VVU), huduma za afya kwa ujumla hasa kwa kinamama
wajawazito na watoto na kuimarisha mifumo ya taasisi katika sekta hiyo.
Fedha
zilizopatikana kwenye harambee hiyo zilitolewa na watu mbalimbali baada
ya kuhamasika na kuguswa na jinsi Taasisi ya Mkapa inavyowasaidia na
kuokoa maisha ya Watanzania wengi hasa maneo ya vijijini.
Mgeni
rami kwenye harambee hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho ambaye alishirikiana na maraisi
wastaafu, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na Benjamini William Mkapa.
Vitu
mbalimbali vilinadiwa kwenye harambee hiyo zikiwepo picha za maraiasi
hao walioingoza Tanzania kwa awamu tofauti tangu mwaka 1985.
Kabla
ya kuanza mnada huo, tayari watu binafsi, mashirika na kampuni
mbalimbali zilikuwa zimehamasika na kuchangia shilingi bilioni 1.5
ambazo zilikuwa ni nusu ya makadirio.
Mmoja
wa wahamasishaji na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahamani
Kinana amesema Mheshimiwa Mkapa amekuwa akishawishi wahisani wa nje
waisaidie taasisi hiyo kufanikisha mikakati yake lakini safari hii
ameona ni vyema Watanzania wenyewe wakachangia. Hali hiyo akaielezea
itatia hamasa zaidi na kuonyesha moyo walio nao wananchi katika
kuchangia maendeleo yake.
Ofisa
Mtendaji wa Taasisi ya Mkapa, Dk Ellen Senkoro ametoa maelezo mafupi
kuhusu taasisi hiyo, kazi inazofanya na kusudio la harambee.
Amesema
kuwa mchango huo wa hisani wa shilingi bilioni 3 ni bajeti ya mwaka
mmoja katika kutekeleza mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuchangia
jitihada za serikali kupambana na janga la Ukimwi, kuzuia vifo vya
kinamama na watoto ili kutimiza malengo ya milenia namba nne, tano na
sita. Mradi huo mzima utagharimi shilingi Bilioni 15.
Amesema
Taasisi ya Mkapa tayari imejitanua na ina wanawafanyakazi waliosambaa
nchi nzima jambo ambalo linampa moyo kuwa watafanikisha lengo
walilokusudia kwenye kipindi hicho cha miaka mitano.
Mheshimiwa
Rais Kikwete amekiri kwenye harambee hiyo kuwa pamoja na juhudi kubwa
za serikali za kuimarisha huduma za afya nchini, bado huduma hizo
hazijafikia kiwango kinachotakiwa kama inavyopendekezwa kitaalam.
Akaisifu
Taasisi ya Mkapa kwa juhudi zake za kupunguza tatizo hilo huku
akiwahamasisha watu mbalimbali waliohudhuria kuchangia ili kuleta
matumaini kwa Watanzania, hasa waishio vijijini.
“Tunaihitaji
sana Taasisi ya Mkapa na ufanikishaji wa miradi yake unategemea kujitoa
kwenu katika kuichangia,” amesema Mheshimiwa Rais Kikwete.
Watu binafsi, mashirika, kampuni na taasisi mbalimbali zilishiriki kwenye chakula hicho cha hisani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Benjamini Mkapa kuendesha harambee kwa kuhamasisha Watanzania kuichangia.
Taasisi ya Makapa ni nini?
Taasisi
ya Mkapa ni mfuko wa fedha wa kuendesha miradi ya afya kwa kuzingatia
huduma kwa jamii bila kutegemea kuzalisha faida. Ilianzishwa Aprili
2006 kwa lengo la kusaidia juhudi za Serikali katika kuwaletea
Watanzania maendeleo.
Huu
ni mradi ambao ulibuniwa na Watanzania kwa ajili ya kuboresha maisha ya
Watanzania hasa wanawake, watoto na wa wale waishio na VVU.
Tayari
Taasisi ya Mkapa imemaliza miradi ya awamu ya kwanza na sasa wanaanza
ya pili. Inagwa walianza katika mikoa michache katika miaka mitano
iliyopita tangu ilipoamzishwa mwaka 2006, tayari miradi yake imeenea
nchiyetu
Comments
Post a Comment