DOGO JANJA ATIMULIWA TIP TOP CONNECTION


 
Nyota wa muziki wa kizazi kipya  kutoka  ‘kruu’ ya  Tip Top Connection  yenye maskani yake pande za  Manzese  jijini  Dar  es  Salaam  Abdul Abubakar Chende ‘Dogo  Janja’  ametupiwa  virago   ndani ya kundi hilo.
 
Akizumngumza na  mpekuzi wetu mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally  ‘Madii’  amesema kuwa  Dogo Janja  ameshindwa  kuendana na  makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo  kuhudhuria  shuleni kama alivyokuwa akitakiwa  kufanya kila siku  badala yake  amekuwa akiendekeza  starehe na  wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.

“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa  maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya  kurudi kwao  na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake  kumuarifu kuwa Tip Top   hatuko na mwanae kwa sasa”  alisema Madii

Katika hatua nyingine Madii  amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na  kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi  kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa  na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega shule na kwenda kujificha  nyumbani kwa TundaMan  huku akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.

Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na mara moja  kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda  kumsaka,  lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha  uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya  alikanyaga  kuku  na  siri yake kujulikana kuwa amejificha hapa na  ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho chake  tayari kurejea ‘kileji’.

"vimekuwa ni vitendo vya kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA