TBL YATOA SH. MIL 53 KUSAIDIA MRADI WA MAJI CHUO KIKUU CHA ST AUGUSTINE
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Steve Kilindo (katikati), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
sh. milioni 53, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha St. Augustine (SAUT)
Mwanza, Taaluma, Padri Thadeus Mkamwa (kulia) katika hafla iliyofanyika
chuoni hapo hivi karibuni. Anayeshuhudia kushoto ni Naibu Makamu
Mkuu wa chuo hicho Utawala na Fedha, Padri Peter Mwanjonde. Msaada huo
ni kwa ajili ya mradi wa maji chuoni hapo pamoja na kilimo cha
umwagiliaji.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve
Kilindo, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT, Mwanza, kabla
ya kukabidhi mfano wa hundi yenye themani ya shilingi milioni 53
fedha ambazo zimetolewa ili kutekeleza mradi wa maji kwa matumizi ya
wanachuo na kilimo cha umwagiliaji.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St. Augustine ( SAUT) Taaluma,
Padri Thadeus Mkamwa, (mwenye koti jeusi) akizungumza na wanafunzi na
walimu wa chuo hicho muda mfupi kabla ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya
shilingi milioni 53 kwa ajili ya mradi wa maji na kilimo cha
umwagiliaji. Hundi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia Tannzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kutoka kulia)
jijini Mwanza hivi karibuni. Mwenye miwani ni Naibu Makamu Mkuu wa
chuo hicho , Utawala na Fedha, Padri Peter Mwanjonde .
Comments
Post a Comment