BAADA YA FISHCRAB, PRODUCER LAMAR AJA NA FILMATIC


Producer na mshindi wa tuzo za Kili Lamar wa Fishcrab ameamua kuonesha kuwa si uandaaji wa muziki pekee anaouweza bali kamba yake ni ndefu zaidi ya hapo ilipomfikisha.


Mpishi huyo wa midundo ya ukweli nchini, amefungua kampuni mpya chini ya himaya yake ya Fishcrab iitwayo Filmatic.

Akiwa muongozaji mkuu na mchukua picha, mpaka sasa Lamar na timu nzima ya Filmatic ameshatengeneza video tano.

Jana kupitia ukurasa wa Twitter alisema amemaliza kushoot video ya wimbo mpya wa rapper Jaffarai uitwao ‘Tembea Nami’ aliomshirikisha ndugu yake wa Kenya mwanadada Naziz.

“Done filming farrai n naziz neu vid tembea na mi can’t wait the edit n color grade!” alitweet.

Kuhusu Filmatic kujiingiza kwenye utengenezaji wa filamu, Lamar amesema hiyo itategemea kama akipata bajeti ya kutosha.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA