WAREMBO WA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012 WATAMBULISHWA WAKATI WA UZINDUZI WA BENDI YA SKYLIGHT NDANI YA MAFIAN LOUNGE JIJINI DAR


Mratibu wa Shindano la Miss Dar Intercollege 2012, Dina Ismail akiwanadi warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 wakati wa uzinduzi wa bendi ya SkyLight ndani ya Mafian Lounge jijini Dar es Salaam wikendi iliyopita. 
 Wakifunguliwa shampeni kwa nderemo na vifijo.


Baadhi ya Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiwamejipanga mbele ya wadau na wadhamini katika uzinduzi wa bendi ya SkyLight iliyofanyika  Mafian Lounge iliyopo Masaki, bendi hiyo inamilikiwa na mmoja wa wadhamini wao Ndege Insurance.

Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.

Alisema mpaka sasa warembo 15 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus, Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.

Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.

“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA