BSS kuanzia rasmi Dodoma



Ziara ya kusaka watu watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma mwezi huu wa Juni tarehe 15 katika Ukumbi wa Royal Village. 

Akizungumzia ziara hiyo bosi mkuu wa kampuni waandaaji Benchmark Production, Ritha Paulsen amesema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.

Kampuni yake inatarajia kuchukua vijana wenye vipaji watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakao kuwa wawakilishi wa Dodoma katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam. 


Alisema kuwa wakiwa mkoani, wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa BSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo. 

“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim,hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha.

Madam Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama Jabir pamoja na Master Jay

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA