Maafisa mawasiliano na mahusiano kutoka taasisi mbalimbali na wizara za serikali jana walitembelea chuo kikuu cha mt.Augustino-Mwanza.Maofsa mawasiliano hao ambao wamekuja Mwanza kwenye kikao chao ambapo kinawakutanisha PROs Takribani 50 kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Ziara yao ya kuja SAUT ilikuwa na lengo la kuja kujionea ni kwa jinsi gani chuo kimepiga hatua tangu maafsa hao wahitimu miaka ya hapo nyuma, takribani asilimia 98 ya Maafisa hao wamesomea chuo hiki cha SAUT katika shahada ya kwanza,na shahada ya Uzamivu lakini pia waliambatana na maafsa habari wengine pia ambao wamesomea vyuo tofaut hapa nchini.
Maafsa mawasiliano na uhusiano hao waliweza kukipongeza chuo hiki kwa hatua mbalimbali wanazozichukua katika uboreshaji wa miundombinu, pia na mikakati mizuri kabisa ya kielimu,lakini pia waliweza kukipongeza chuo kwa kutokupandisha ada tangu wao wamalize takribani miaka 8 iliyopita hadi leo ada imebaki kuwa palepale, hivyo chuo kimejidhatiti kuwakomboa kielimu wanafunzi wanaotoka katika familia yenye vipato vya chini
|
Makamu mkuu wa chuo Charles Kitima akiwasili eneo la tukio |
Comments
Post a Comment