VIDEO YA "LALA SALAMA" YA DIAMOND IKO NBIONI KUTOKA

Ujumbe mahsusi uliomo kwenye wimbo unaowasilishwa kwa sauti tamu, yenye upendo uliozungukwa na uchungu na kusindikizwa na ala nzuri, ni sababu zilizoufanya wimbo huo upendwe na watu wa kila rika.
Lala Salama, wimbo unaobeba jina la albam ya pili ya Diamond Platnumz umehit mtaani bila hata kuachiwa redioni.

Si jambo la kushangaza kumsikia mtoto mdogo akiuimba wimbo huo mstari wa kwanza hadi wa mwisho bila kukosea.

Lakini kwa wanaume ambao wamewaacha wake ama wachumba zao vijijini/nyumbani na kwenda kutafuta maisha mjini, wana kila sababu za kuupenda wimbo huo kwakuwa unaziwakilisha hisia na mawazo waliyonayo juu yao (familia) na jinsi wanavyohangaika mjini.

Na sasa Diamond ameanza kushoot video ya wimbo huo ambao ni muendelezo wa wimbo wake uitwao Nitarejea aliomshirikisha mwanadada Hawa.

Nitarejea ni wimbo uliyoyagusa maisha ya wengi akiwemo Mheshimiwa Zitto Kabwe ambaye juzi alimuuliza swali, “nini kilikuwa kwenye mawazo yako ktk wimbo wa #NITAREJEA ? Whats the story behind? Whats the thinking behind?

Diamond alijibu, “Dah! Ni Mungu tu mkuu,ila niligundua wanaume wengi wa mikoani huja Dar na wa Dar huenda nje za nchi kutafuta Maisha na kuacha familia.”

Mheshimiwa Kabwe akachombeza, “Halafu hawarudi. Nataka kuona ubunifu wako after that. ‘Nimerejea’ au ‘sikutaki tena!

Ndipo Diamond kupitia swali hilo akawapa habari njema wapenzi wa ‘Lala Salama’ kuwa video ipo mbioni kuja kwa kumjibu Mhe.Kabwe, “LOL! Ipo tayari inaitwa “LALA SALAMA” ni muendelezo wa Nitarejea ambayo nashut Video sasa, Ntakutumia BBM uiskie”

Bahati nzuri Zitto Kabwe ameshaisikia LALA SALAMA na tunaamini kausikia ubunifu wa mshindi huyo wa Tuzo za Kili.
Kwa ratiba ngumu aliyonayo msanii huyu mwenye mafanikio makubwa katika kipindi kifupi cha career yake inayohusisha show, kurekodi, kushoot video, mahojiano na vyombo vya habari na maisha binafsi, hatushangai akiandika, “Been soo busy dah, I think I need a vacation!


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA