NMB YATOA MAFUNZO KWA VYAMA VYA USHIRIKA TARIME
- Get link
- X
- Other Apps
NA Shomari Binda
Tarime,
...
Benki ya NMB tawi la Tarime imeendesha mafunzo kwa vyama vya msingi vya
ushirika yanayohusu namna ya kutumia stakabadhi ya mazao ghalani katika
maandalizi ya ununuzi wa zao la kahawa katika msimu mpyaunaotarajiwa
kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa.
Akifungua mafunzo hayo kwa
niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Katibu tarafa wa Kata ya Inchage Machango
Jonathani alisema hiyo ni fursa pekee kutoka katiuka benki hiyo katika
kuwapa mafunzo viongozi hao kabla ya kuingia katika msimu wa manunuzi
ya zao hilo na kuwataka kwenda kueneza elimu hiyo kwa wakulima
mashambani.
Alisema mfumo huo wa stakabadhi ya mazao ghalani
unaotumiwa na benki ya NMB unamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kwa
bei iliyo nzuri na kupata malipo yake bila kuzungushwa hivyo wakulima
wakifikishiwa taarifa zilizo nzuri watautumia mfumo huo.
Meneja wa kanda wa mfumo wa mazao ghalani wa benki ya NMB Samwel Msote
alisema wameamua kuyatoa mafunzo hayo mapema ili kuwajengea uwezo
viongozi hao wa vyama vya msingi vya ushirika Wilayani Tarime ili
kuwepo na ufanisi zaidi katika ununuzi wa msimu huu na kuvuka lengo.
Alisema katika msimu wa mwaka jana licha ya kutengwa fedhs nyingi kwa
ajili ya mfumo huo vipo vyama vya ushirika ambavyo vilishindwa
kuzitumia kwa kufanya manunuzi huku vingine vikifanya manunuzi kidogo
ya kahawa na kuwataka viongozi hao kujipanga mapema hili msimu huu
vyama hivyo viweze kununua zao hilo kwa wingi.
Alkidai kahawa
ya Tarime katika msimu uliopita ilikuwa nzuri na yenye ubora na
kupitishwa na bodi ya kahawa Tanzania na kuwaomba viongozi hao kuendela
kuwahamasishwa wakulima jinsi ya utunzaji wa zao hilo hili liweze
kupata ubora zaidi.
Kwa upande wak meneja wa benki ya NMB tawi
la Tarime Amosi Daniel aliwataka viongozi hao wa vyama vya ushirika
kufungua accaunti ya busines accaunti kwani ndio accaunti pekee
inayotumika katika malipo ya stakabadhi ya mazo ghalani na kuwataka
kuwa makini katika uandikaji wa Hundi za malipo.
Naye Katibu
wa chama cha ushirika cha Bungerere Lucas Masa alisema huo ni mfumo
mzuri unaoendeshwa na benki hiyo ya NMB kwa kuwa unamuwezesha mkulima
kuweka mazao ya ke ghalani na kupata mkopo ambao unamuwezesha kutatua
matatizo mbalimbali na kuharakisha shugfhuli za maendeleo.
Aidha katibu huyo aliiomba Serikali kwa kupitia maafisa ugani
kuhakikisha wanafika kwa wakulima vijijini na kuwa na ushirikiano wa
karibu na vyama vya ushirika ili kuweza kubolesha zao la kahawa kwa
kuwa tayari Wananchi wa Tarime wameshapata mwitikio mkubwa juu ya zao
hilo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment