DIAMOND: "NAMSHUKURU WEMA SEPETU KWA KUNIFUNDISHA KIINGEREZA"

Diamond akiwa katika studio za Clouds FM kwa ajili ya interview.
---
Kwenye kipindi cha XXL jana kinachorushwa na Clouds Fm msanii Diamond aliulizwa ni kwa vipi aliweza kujielezea vizuri sana kwa lugha ya Kingereza baada ya performance yake kwenye Big Brother StarGame maana wengi huwa wanashindwa ifikapo hatua hiyo Diamond alifunguka na kukiri kwamba mrembo Wema Sepetu amechangia kiasi kikubwa kwake kujua lugha hiyo na kusema napenda kumshukuru 'WEMA ENGLISH COURSE'...... kusema ukweli nilifurahi sana kusikia hivyo maana pamoja na mascandal yao yote angalau Diamond ameweza kuongelea upande mzuri wa Wema na ni jinsi gani ameweza kuchangia mafanikio yake kwa kiasi fulani.

Wakati huo huo Diamond pia ameongela tour yake ambayo anatarajia kuifanya nchini Marekani baadae mwaka huu na nyumba anayo jenga Tegeta ambayo amekiri mpaka sasa ametumia karibia Tshs milioni 69. Nyumba ni ya kisasa, ina vyumba vya kulala vinne, vitatu vyote master, kuna studio, jiko, choo, bafu nk. Pamoja na nyumba hiyo kuna zingine pia ambazo hakupenda kuongelea ila I hope and I'm sure kuna siku atafunguka.

Tunapenda kumtakia kila la kheri Diamond na Big Up to mrembo Wema Sepetu kwa msaada alio mpatia Diamond kwa kumfundisha Kingereza.

source www.freebongo.blogspot.com



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA