Big Brother yaifunga akaunti yake ya Youtube kutokana kutumiwa vibaya



Akaunti maalum ya Youtube iliyokuwa ikitumiwa kuweka video za Big Brother imefungwa kutokana na matumizi yasiyo halali ya video zake.


Uamuzi huo utawaamiza watu wengi waliokuwa wakitegemea kujua kinachoendelea kwenye mashindano hayo na ambao hawaipati channel maalum ya TV inayoyarusha moja kwa moja (live).

Akaunti hiyo rasmi ilifunguliwa tarehe 5, May 2012 mashindano hayo yalipoanza.

Hata hivyo video zote za BBA Stargame zitaendelea kupatikana kwenye blog ya Big Brother inayomilikiwa na DSTV pamoja na akaunti zingine zisizo rasmi kwenye mtandao wa You Tube.

Uamuzi huo umechukuliwa kama njia ya kuzuia uharamia, kuzuia downloads zisizo halali na matumizi ya kibiashara nje ya channel rasmi za Endemol Productions, ambayo ndio waandaaji wa Big Brother Africa.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA