GODZILLA AWARUSHA WANASAUT USIKU WA KUAMKIA LEO

Usiku wa kuamkia leo imefanyika bonge moja la show inayofahamika kama Gala nite kwa ajili ya kuondoa stress za hapa na pale kwa wanafunzi kabla hawajaanza mitihani ya mwisho ya semister ya pili. 

Before mkali Godzillla hajapanda kulikuwepo na show za hapa na pale kama hip hop battle kutoka kwa wasanii wanaopatikana hapa SAUT na wengine wanaochana R&B na wakali kibao kutoka chuggaaaa......pia kulikuwepo na mchezo wa pool table

Godzilla kutoka hood ya Salasala jijini Dar,mkali huyu wa free style alipanda usiku wa saa 6 huku mashabiki wake wakimsubiri kwa hamu kubwa wengine wakidhani kuwa ni changa la macho kwani walidhani itakuwa show ya kitoto msanii kupanda saa 4 usiku lol.....basi wakati kapanda jukwaani tu kelele za kutosha zilisikika kutoka kwa mashabiki wake,ambapo show ilifanyika kwa takribani dakika 45 bila kupumzika. Zilla aliweza kuwarusha mashabiki wake mpaka anashuka kwenye jukwaa mashabiki wake bado walikuwa hawajakata kiu hasa pale alipoanza kupiga free style za kuchana mambo mbalimbali
Godzilla kutoka sala sala akiwarusha mashabiki wake waliopo chuo cha SAUT

Dj akishangaa wakati Godzilla akimchana kwa free style
Mrope and Mahera wakatokelezea

Godzilla akishambulia jukwaa usiku wa gala NITE

NYOMIIIIIIII

Binya mkali wa R&B akiwarusha mashabiki wake

wakali wa free style Shynner (L)kutoka LLB na MB man wanaopatika chuoni SAUT

Mheshimiwa waziri wa wizara ya Utalii na Burudani kutoka serikali ya Wanafunzi SAUTSO naye akachana kidogo

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA