HAWA NDO MAFREEMASON WALOTINGA CLOUDS FM MAPEMA LEO
Pichani ni Dkt. Kemu Mzee
(kushoto) na Alhaj Prof. Dkt. Salim Kungulila (kulia) wanaojiita
Freemasons walio temebele kituo cha Clouds FM leo asubuhi kwenye
kipindi cha Leo tena na kuelezea ufreemason wao
Hapa Alhaj Prof. Dkt. Salim
Kungulila kutokea Magomeni Mikumi Dsm. Ni mwalimu wa dini mbali mbali.
Pichani akielezea ancho jua kuhusu ufreemason na namba 666 ambapo
alishindwa kukiri ufreemason wake bali alismea yeye ni MuaashiHuru
Hahaha huyu ndiye Dkt. Kemu Mzee ambaye yeye alijieleza akasema ni mganga wa tiba asilia na ni Freemason wa Kisukuma.
---
Wanadai
wao wanafundisha dini zote na kudai kua kila mtu duniani ni Freemason
na pia wafafanua maana halisi ya ufreemasons ila mwisho wasiku
walishindwa kujibu kama wao ni mafreemasons au laaah! Wakaishia kusema
wao ni WaashiHuru…
Walipo ulizwa kama freemason wanaabudu shetani wakashindwa kujibu.
Dkt.
Kemu Mzee alisema ufreemason ni kitu ambacho hukioni na ni kama kuuza
bidahaa haraka haraka kabla ya mwenzio so hapo wewe uliye uza haraka
haraka ndo unatajirika haraka.
Walipo
ulizwa juu ya masharti ya kujiunga waksema yanapatikana ofisini kwao na
ni lazima mtu apate matibabu yao ambayo ni lazima na kuongezea ni sawa
na kujiunga na chama fulani ukafuata masharti yao so kwa upande wao
tiba yao ndo lazima.
Na Alhaj Prof. Dkt. Salim alisema
watu wanapo ambiwa majini wanaogopa lakini watu wasihofu maana majini
ni kama mashine. Mpaka sasa sielewi alimaanisha nini hahaha!!!
Kwa
kumalizia waliulizwa kama freemason wanatakiwa kutoa sacrifice (kafara)
ya ndugu wa karibu wakasema sacrifice (kafara) kila mtu anatoa wakristo
au waislamu. Hiyo yakutoa watu ni uzushi pengine.
Hahaha
hakuna siku nimecheka kama leo maana hawa jamaa nahisi walienda kuuza
sura walikuwa wanapiga chenga maswali na kujibu yao tu.
Kwa hiyo kuconclude na kutokana na maelezo yao wao wamejiita WAASHIHURU tafsiri yake FREEMASON!
Picha kwa hisani ya TeenTZ
Comments
Post a Comment