vitambulisho vya Taifa si mbadala wa kadi ya mpigakura

MWENYEKITI
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa,
Damian Lubuva amesema vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) si mbadala wa kadi ya mpiga kura.(Martha Magessa)
Kauli
hiyo aliitoa jana kwenye mkutano na viongozi wa vyama vya siasa
alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyetaka kupata ufafanuzi wa
vitambulisho vipi vitatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Lipumba
alinukuu kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa
vitambulisho vya taifa kuwa vitambulisho hivyo vingetumika kwenye
shughuli za uchaguzi.
Lubuva alisema sheria iliyopo bado inatambua kadi ya mpiga kura kutumika kwenye chaguzi na kura za maoni ya katiba mpya.
“ Si kama
napingana na Rais (Jakaya Kikwete), siku ile nilikuwepo na rais alikuwa
akielezea faida ya kitambulisho cha taifa na kusema ‘pia vitatumika
katika shughuli za uchaguzi. “Hii ina maana kama mtu kapoteza kadi ya
mpiga kura, kitambulisho cha taifa kitamsaidia kutambulika. Naomba
nieleweke kuwa vitambulisho vya Nida si mbadala wa kadi ya mpiga kura
ila vitasaidia wakati wa uchaguzi.
Lubuva
aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kusaidia katika kuhamasisha
wananchi kujiandikisha katika shughuli za uboreshaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura ili kazi iwe rahisi.
Hata
hivyo, hoja iliibuliwa na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo waliodai
kuwapo kwa zuio la kufanya mikutano na kupendekeza muda wa uandikishwaji
uongezwe.
Chanzo:Habarileo
Comments
Post a Comment