WAANDISHI WA HABARI MWANZA WATEMBELEA SAHARA MEDIA GROUP LEO

Mkurugenzi wa Sahara Media Group bw. Anthony Dialo akiongea na waandishi wa (habari wataonekana katika picha nyingine) ambapo amesema kuwa kuanzia mwezi Septemba 2012 minara na mitambo ya king'amuzi kipya itawashwa rasmi kwaajili ya kuanza kufanya kazi. Star Tv pamoja na televisheni zote za IPP zitaingia katika mfumo wa digitali kupitia king'amuzi hicho.

Serikali kupitia Tume ya Mawasiliano nchini imesema kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka 2012 ndiyo itakuwa mwisho kwa vituo vyote vya televisheni kurusha mawasiliano yake katika mfumo wa analogy na kujiunga na mfumo wa digitali, hivyo basi kwa msingi huo kampuni ya Sahara Media Group na wadau shirika wako kwenye mchakato kuharakisha zoezi la kusimika minara na mitambo kwaajili ya kuingia kwenye masafa bora ya kisasa.

Wadau wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliopata mwaliko kutembelea Sahara Media Group na harakati za usimikaji mitambo mipya.

Ujenzi unaendelea katika eneo la juu ghorofa lenye shughuli mbalimbali za Sahara Media Group, pichani ni ukumbi utakao husika na makusanyiko ya aina yoyote kwaajili ya kutengeneza vipindi mbalimbali kwa kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa Sahara Media Group bw. Anthon Dialo akifafanua jambo kuhusu moja ya vyumba vya habari na urushaji wa vipindi upande wa kituo cha televisheni Star Tv, ambapo kwa sasa vyumba vimeongezwa zaidi kwaajili ya kutoa fursa kwa vipindi vingi kutengenezwa kwa wakati mmoja.

Hapa ni katika chumba cha urushaji matangazo ya Televisheni Star Tv Mwanza.

Wadau wa habari na vipindi mbalimbali Star Tv wakiwa shughulini kukusanya matirio na kuandaa vipindi Star Tv Mwanza, mchekshie braza Abdalah Tilata....

Kazi ya kuhariri vipindi inaendelea....

Waandishi wa Habari tulipata fursa ya kutembelea karakana ya kuhifadhi vifaa kwaajili ya ujenzi wa minara madhubuti pamoja na kujionea mitambo mipya ya ureshaji wa matangazo kwa mfumo wa digitali.

Hakika ni uwekezaji mkubwa.

"Uzuri wa mfumo wa digitali kupitia kingamuzi unakupa fursa ya kupata chanel nyingi zaidi katika frequency moja, Inakupa afya ya macho kupata picha safi kwa matukio na taarifa mbalimbali" says Mr. Dialo.

"Jumla ya leseni tatu zilitolewa na TCRA kwa ajili ya kurusha matangazo ndani ya mfumo wa digitali, TBC wakishirikiana na Star Media wanakingamuzi chao kiitwacho Startimes, Makanisa wakishirikiana na Agape wanaking'amuzi chao kiitwacho Ting, na leseni ya tatu ilitolewa kwa Sahara Media Group wakishirikiana na IPP,  hivyo kaa tayari kujionea mapinduzi mapya ndani ya mfumo wa Digitali"  Aliongeza Mkurugenzi huyo wakati wa mahojiano yaliyofanyika kwenye minara ya urushaji wa matangazo iliyopo katika vilima vya Nyanshana wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.. 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA