MWILI WA MAFISANGO WAAGWA NA WATANZANIA
Wachezaji wa timu ya Taifa la Tanzania iliyoteuliwa hivi
karibuni, mbele ni Juma Nyoso (L) na John Boko (R) wakiwa wamebeba
jeneza la mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba marehemu Patrick
Mafisango, kwaajili ya kuagwa katika viwanja vya TTC Chang'ombe jijini
Dar es salaam nchini Tanzania.
Mwili wa marehemu ukiwasili viwanjani hapo kwaajili ya wadau mbalimbali
kutoa heshima zao za mwisho, mbele wanaonekana Juma Nyoso na John Boko
na kwa nyuma ni Shahbani Nditi.
Kombe la Ubingwa Tanzania Bara likiwa limewekwa juu ya jeneza la
marehemu Patrick Mutesa Mafisango aliyezaliwa mwezi March mnamo mwaka
1980 na kufariki dunia tarehe 17 May 2012.
Sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania wakiwa na
majonzi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mchezaji wa Simba
aliyefariki dunia Patrick mafisango.
Golikipa wa Simba na Taifa Stars Juma Kaseja alishindwa kujizuia
kulia hali iliyosababisha kupatiwa msaada toka kwa marafiki
waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango.
Mafisango, alikuwa amechaguliwa kuchezea kikosi cha
kitakachowania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya
Algeria alifariki katika ajali ya barabarani asubuhi ya kuamkia jana
mjini Dar es Salaam Tanzania katika ajali iliyohusisha pikipiki na gari
wakati gari alilokuwa akiliendesha lilipoteza mwelekeo na kuanguka
kwenye mtaro..
source www.gsengo.blogspot.com
Comments
Post a Comment