UFUNGUZI WA SAUT BUSINESS INCUBATION CENTRE
Kesho tarehe 31/05/2012 kuanzia saa 8:00 Mchana- 11:30 katika ukumbi wa M12 katika chuo kikuu cha Mt.Augustino kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kituo cha ujasiliamali kitakachojulikana kwa jina la BUSINESS INCUBATION CENTRE (B.I.C).
Centre hii ni mahususi kabisa katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanafunzi wote wa SAUT ambao watakuwa mwaka wa mwisho wa masomo yaani mwaka wa 3 na 4,baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho wa semister watapata fursa ya kuweza kupata mavunzo ya ujasiliamali kwa muda wa miezi 3 BURE kabisa,ambapo chuo kimejitolea kutoa majengo yake,kuleta walimu kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi.
Dhumuni la kuanzisha Centre hii ni kuweza kuwasaidia hususan wanafunzi
wa SAUT na jamii kwa ujumla njia tofauti tofauti za kuweza kupata fursa za kujiajiri wao
wenyewe kwa kuanzisha makampuni yao na pia kuweza kuwapatia mwanga juu ya
jinsi gani wanaweza kutumia malighafi zilizopo nchini na kuweza
kumiliki njia kuu za uchumi kwa maendeleo ya jamii na pia kwa nchi kwa
ujumla badala ya kuwategemea wawekezaji waweze kushikilia njia hizo
wakati wanazuoni wapotele hapa nchini huku wakiangaika kwa kutembea na Bahasha mkononi wakiomba ajira katika makampuni na ofsi mbalimbali hapa nchini.
Center hii itakuwa endelevu,hivyo basi wanafunzi wote wa kutoka kozi zote za hapa SAUT wanaomaliza masomo yao wanaombwa kuchangamkia nafasi hii ya kipekee kabisa kuweza kutokea hapa SAUT na ndani ya vyuo vya hapa nchini,pia wajasiriamali wa hapa nchini waliofanikiwa watapata fursa ya kuweza kutoa ushuhuda wao ni kwa jinsi gani wameweza kufikia malengo yao waliokuwa wamejiwekea na hatua ambazo wamezitumia mpaka hapa walipofikia,nia ni kuweza kuleta uhalisia halisi kwa wanafunzi hao wakati wa mafunzo. mafunzo haya yatakuwa yamejikita zaidi katika vitendo.
kwa wale wanafunzi watakaoweza kufanya vizuri kwa kuja
na michanganuo ya kibiashara (Business plan) zao zitakazokuwa zimeandaliwa vizuri, basi baada ya
masomo chuo kitaweza kuwawezesha kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya
kuanzisha biashara zao.
Vyombo vya habari,makampuni ya kibiashara mnakaribishwa sana katika uzinduzi huu.
Mnakaribishwa nyote.
Comments
Post a Comment