NGORONGORO YAING'OA SUDAN, ULIMWENGU SHUJAA

Ulimwengu, mfungaji wa bao la Ngorongoro
 

 

 

 

 

Timuya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika usiku huu, baada ya kutioa Sudan kwa jumla ya mabao 4-3.

Ngorongoro leo imekubali kichapo chepesi cha mabao 2-1 ugenini, kwenye Uwanja wa Khartoum, baada ya awali kushinda 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na sasa itachuana na Nigeria Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikicheza Julai 28, mwaka huu Dar es Salaam.
Sudan walipata mabao yao kupitia kwa Mohammed Abdelrahman dakika ya 10 na Ahmad Nasr kwa penalti dakika ya 65, wakati bao la Ngorongoro lilifungwa na mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu kabla ya mapumziko.
Ngorongoro Heroesinatarajiwa kurejea nchini Jumapili (leo) majira ya Saa 3 asubuhi.
Mshindi kati ya Ngorongoro na Nigeria atamenyana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Kongo Brazzaville, mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu ugenini na marudiano Oktoba 6.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA