BANDA LA TANZANIA LA UTALII LAZIDI KUFANYA VIZURI INDABA- NCHINI AFRIKA KUSINI
Naibu
Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa (watatu kushoto)
pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji Biashara na viwanda wa Afrika Kusini
Bibi Elizabeth Thabethe (wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na
baadhi ya waoneshaji kutoka Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki (wan ne
kushoto) alipotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA
mjini Durban Afrika Kusini.
Banda
la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya INDABA
yanayoendelea jijini Durban Afrika Kusini limeendelea kuvutia viongozi
na watu wa kada mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini
wanaotembelea maonyesho hayo.
Miongoni
mwa waliotembelea banda hilo shindwa kuzuia hisia zao hususan kwa
maelezo na vielelezo vinavyoonesha uzuri na upekee wa vivutio vya
utalii vya Tanzania na shughuli za utalii zinavyoendeshwa nchini ni
Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa na
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Viwanda na Biashara la Afrika Kusini Bibi
Elizabeth Thabethe ambao kwa pamoja walitembelea Banda la Tanzania na
kujionea vielelezo mbalimbali sambamba na kupata maelezo
yaliyowafurahisha sana kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza
na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk Aloyce Nzuki
na waoneshaji wa Tanzania kwa ujumla Naibu huyo waziri alifurahishwa na
kuvutiwa na jinsi Tanzania kupitia Bodi ya Utalii ilivyojipanga katika
kuitangaza Tanzania duniani na jinsi ambavyo Tanzania imekuwa ni
mshiriki mzuri wa maonesho ya INDABA na kukiri kuwa Tanzania imekuwa
ikitoa changamoto kubwa kwa nchi nyingine wanachama wa SADC katika
sekta ya Utalii. “Tanzania ni nchi tishio katika sekta ya utalii
miongoni mwa nchi za SADC, ni nchi inayonivutia sana “ alisema Bibi
Tokozile Xasa
Jumla
ya makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za serikali
zinashiriki katika maonesho hayo ambayo ni makubwa kuliko yote barani
Afrika. Maonesho haya hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini.
Katika maonesho kama haya mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa
tuzo ya kuwa Banda Bora kuliko yote katika maonesho hayo miongoni mwa
nchi za SADC.
source www.freebongo.blogspot.com
Comments
Post a Comment