Lowassa atatua mgogoro wa Mwekezaji na Wananchi wa Meserani

Picture
Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa akizungumza na wananchi (wafugaji) wa Kijiji cha Nararami Kata ya Meserani, kwa muda mrefu wafugaji hao wamekuwa na mvutano na mwekezaji wa shamba Abraham. Mgorogo huo umetajwa kuwa kwenye shamba lenye Hekari 4,100 ambazo zipo ndani ya chanzo cha maji kinachotumika wakati wa kiangazi kunyweshea mifugo na malisho.
Picture
Mwekezaji akiwa kwenye mkutano wa usuluhisho uliokuwa ukiongozwa na Mbunge Edward Lowassa. Hata hivyo baadhi ya wafugaji hao wa Kimaasai waligoma kukaa karibu na mwekezaji huyo wakidai amekuwa akiwanyanyasa na kuua mifugo yao, pembeni yake ni kijana wa Kimaasai akiwa ameusimika mkuki wake chini huku kikao kikiendelea.
Picture
Baadhi ya watu wakiwamo akina mama wa kabila la Wamaasai wakimpongeza Edward Lowassa kwa hatua ya kumaliza mgogoro huo baada ya kupendekeza mwekezaji huyo atafutiwe eneo jingine la kulima na eneo lenye chanzo cha maji alirudishe kwenye serikali ya Kijiji.
Picture
Baadhi ya wafugaji wa Kimaasai wakiwa wamepanda gari la Mwekezaji Abraham ambaye kwenye kikao walikuwa wakidai hawataki hata kumuona kijijini hapo kutokana na kuua mifugo yao kwa madai kuwa aliweka sumu kwenye majani.
 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA