WAZEE YANGA WATOA SIKU SITA KWA NCHUNGA NA WENZAKE KUACHIA NGAZI, KINYUME NA HAPO PATACHIMBIKA

MAMBO ndani ya klabu ya Yanga yamezidi kuitibuka baada ya leo baraza la wazee wa klabu hiyo kutangaza kuwepo kwa mvua ya masika klabuni hapo iwapo mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga na wajumbe wake wa kati ya utendaji hawatojiuzulu kwa hiyari yao kabla ya Mei 20 mwaka huu. Kama hiyo haitoshi, wazee hao wamemtaka makamu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo, Ridhwan Kikwete kusikia machungu kama waliyonayo kwani ni yeye aliyechangia kumleta madarakani Nchunga, “Ridhawan mbona hulii kama wazee wako wewe ulitushawishi kumchangua Nchunga?alihoji Katibu wa baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali. Akizun gumza na waandishi wa habari jana makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga,Akilimali alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na uongozi wa 
Nchunga kushindwa kuongoza na hivyo kuisababishia matatizo mbalimbali.

 Alisema kuwa wameunga mkono maamuzi aliyoyatoa Nchunga ya kutaka kuzungumza nao Mei 20, lakini wanashangazwa na taarifa hizo kwa kuwa aliwakana na kusema katiba ya Yanga haina wazee, hivyo wao wameona siku hiyo iwe ni kwa ajili ya mkutano mkuu wa wanachama wote, huku akiwaomba wanachama kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia Nchunga akijiuzulu. Akilimali alisema kwa mjumbe yoyote wa kamati ya utendaji atakayejiuzulu kabla ya siku hiyo watammthamini, lakini kwa yule atakayeendelea kutaka kubaki madarakani watamuondoa kwa nguvu. “Nchunga alituambia sisi waongo kusema wachezaji wanadai pesa wakati tunatambua kuwa walipoewa shilingi 300,000 ili kuwatuliza na wale ambao anawaita wauza unga.

 “Wanayanga na Watanzania mmewasikia wachezaji wakilia njaa sijui nani ni muongo kati yetu…sisi tulitaka timu kwa maslahi ya Yanga na si vinginevyo,”aliongeza Akilimali “Nchunga kwa maslahi ya Yanga ni vema akaachia ngazi kwani Yanga ikiendelea kuwa chini hapatatawalika waswahili tunasema UKIONA MANYOYA, KALIWA,”aliongeza Akilimali ambaye aliungwa mkono na wazee mbalimbali wa baraza hilo wakiwemo Yusuf Mzimba, Bilali Chakupewqa, Jabir Katundu na wengine. Akienda mabli zaidi, Akilimili alisema baraza hilo limekusanya kiasi cha mil.750 ambazo watazitumia kwa ajili ya kulipa madeni ya wachezaji na wafanyakazi wa Yanga,pamoja na kuzitumia kwa ajili ya usajili wa wachezaji wa ndani na nje ya nchi, pia kutafuta kocha mpya atakayeinoa timu hiyo baada ya Kostadin Papic kumaliza muda wake. Aidha, wazee hao waliwata wanachama wote wa Yanga kutolipa ada ya uanachama ya sh.12,000 kama walivyotakiwa na Nchunga ili kushiriki mkutano huo, pia mjumbe wa bodi ya udhamini Yusuf Manji kuacha kutoa mil.12 kila mwezi na shilingi mil.75 ambazo amekuwa akitoa kwa ajili ya kuendesha klabu, kusitisha zoezi hilo mpaka watakapotangaziwa. “Kama Nchunga hatokubali ombi letu hili kwa madai ya kutokuwa na fedha za kugharamia mkutano siku hiyo aseme ili tushughulike sisi kwa kila kitu kuanzia kutafuta ukumbi na kulipia, usafiri, chakula na mengine kwa ajili ya wanachama toka sehemu mbalimbali nchini ambao watakuwa tayari kushiriki,”aliongeza. Aliongeza kuwa anashangaa klabu hiyo kuwa na hali ngumu ya kiifedha wakati mwenyekiti aliyepita Iman Madega aliacha benki sh.mil.200, kampouni ya Bia Tanzania (TBL) inatoa mi.17 kila mwezi, kadhaliki Manji anayetoa Mil.75 pia kila mwezi lakili fedha zote hizo hazijulikani zinapokwenda.
source: Diana Ismail

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA