RAIS BARACK OBAMA AUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.
Bwana
Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake
wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki
na jamii kwa kutambua uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile
anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia
moja.
Kwa
kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa
za jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa
Marekani. Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu
kuunga mkono ndoa za aina hii.
Rais
Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani
kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao
wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema
wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni
yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za
jinsia moja.
Kauli
ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina
kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa
ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment