MBUNGE ESTER BURAYA ATOA VIFAA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA MANISPAA YA MUSOMA.

Na Shomari Binda
Musoma,

Mbunge wa viti maalumu kupitia vijana mkoani Mara Ester Buraya ametoa vifaa vya michezo kwa kata 13 za Manispaa ya Musoma vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya kuhamasisha michezo kwa vijana na kuibua vipaji ili kuweza kuanzisha ajira za kujitegemea kupitia michezo. 
 Ester amekabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa umoja wa vijana wa CCM kutoka katika kata hizo katika mkutano na viongozi wa matawi na kata uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo na kuhudhuliwa na baadhi ya wadau wa michezo.

Alisema suala la michezo likiwwekewa mkazo na kila mmoja kuna nafasi kubwa ya kuibua ajira kwa kuwa katika dunia ya leo wapo wanamichezo wengi amabo wamefanikiwa na kuwa matajiri wakubwa kwa kupitia michezo mbalimbali hivyo suala la kuhamasisha michezo lina nafasi yake ili kuweza kujenga jamii bora.

Alisema kila kijana ambaye anaona anacho kipaji atumie muda mwingi katika kukiendeleza ili kiweze kumsaidia katika maisha ya baadae na kuacha kujiona mpweke kwa kudai kuwa ukikitumia kipaji vizuri kana nafasi kubwa ya kufanikiwa katika maisha kama ambavyo wanaonekana wanamichezo wengine.

Mbunge huyo wa viti maalumu kupitia vijana alisema ametoa seti moja na mpira mmoja kwa kila kata na hiyo ni mwanzo kwa kuwa ameandaa progaramu maalumu ya kuhakikisha anasambaza vifaa mbalimbali vya michezo katika wilaya zote za Mkoani Mara ili kila mmoja kutokana na kipaji chake aweze kushiriki katika michezo.

Akizungumza na Shomari Binda mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo Ester Buraya alitoa salamu za pole baada ya kupata taarifa ya kifo cha Mhariri wa michezo wa Gazeti la MTANZANIA Rachel Mwiligwa ambaye alifariki usiku wa kuamkia siku ya jumamosi katika hospital ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam.

Alisema alimfahamu Rechal baada ya kukutana naye katika shughuli mbalimbali za kimichezo na kusoma habari zake za michezo na kusema anaungana na wanafamilia,uongozi na Wafanyakazi wote wa kampuni ya New Habari 2006 LTD katika kuomboleza kifo cha Lachel Mwiligwa.

"Nimeumizwa sana na kifo cha Lachel mara baada ya kupata taarifa na huu ni msiba mkubwa katika tasnia ya Habari na wanamichezo wote na wote tulioguswa na msiba huu yatupasa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwa kuwa hii ni mipango ya mungu,tulimpenda lakini yeye aliye juu amempenda zaidi",alisema Estar.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA