Picha za Tamasha la UTAMADUNI WETU v/s BONGO FLAVA
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Dkt. Ibrahim Msengi amezindua tamasha la Utamaduni
Wetu v/s Bongo Flava lililofanyika katika viwanja vya Mandela vilivyopo
katika kata ya Pasua, katika Manispaa ya Moshi ambalo limehusisha nyimbo
mbalimbali ikiwemo za asili, zinazouenzi utamaduni wa makabila
mbalimbali.
Dkt. Msengi amesema moja ya mambo ambayo yanaendelea kuubomoa kama siyo kutokomeza kabisa utamaduni wa Watanzania ni pamoja na utandawazi ambao umekuwa ukichangia wananchi hususani vijana kushabikia tamaduni za Magharibi na kusahau tamaduni za Kiafrika.
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo umuhimu wa waannchi kuendelea kuuenzi utamaduni wao. Akasema, mahali popote utakapokwenda, vitu kama vile lugha, mavazi au chochote kinachokubalika kuutambulisha utamaduni, huwa ndicho kitambulisho husika cha mtu na utamaduni wake.
Naye mratibu wa tamasha hilo, Ismail Mnikite wa Endeleza Foundation amesema lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha, kuendeleza na kuimarisha zaidi utamaduni wetu baada ya kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi.

Comments
Post a Comment