MKUU WA MKOA WA MWANZA AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI MKOANI MWANZA

"Ndugu zangu ila tukumbuke kuwa kama tunadai maslahi bora basi tujuwe uzalishaji wa tija lazima uongezeke tufanye kazi kwa bidii, ubunifu na tija" Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Eng. Ernest Ndikilo akijibu risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Mwanza kwenye sherehe za mei mosi 2012 zilizofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katibu wa kanda TPAWU ambaye pia ni mratibu wa mei mosi Mwanza Cecil Haule akimkabidhi risala mh. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Ernest Ndikilo ambapo kwenye hitimisho risala hiyo imeiomba Serikali sambamba na kupandisha kima cha chini cha mshahara pia imeimba Serikali kupunguza kodi ya mapato kwa Wafanyakazi hadi kufikia asilimia 9 na kwa bidhaa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa mahitaji ya kila siku.
Sherehe hizo zilianza leo asubuhi kwa maandamano na maonyesho ya kusisimua.
Makampuni ya Ulinzi nayo yalinangwa katika hotuba ya mkuu wa mkoa kwani baadhi yao yameshafikishwa mahakamani kutokana na kutowalipa stahiki wafanyakazi wake huku kesi nyingi zikiwasilishwa ofisini kwake.
 
Mfanyakazi Bora toka SAHARA Communication ya jijini Mwanza, wamiliki wa Star TV, Radio Free Afrika, Kiss FM, na gazeti la Msanii Afrika, mpiga picha mr. Maliganya anayepunga mkono akiwa na wadau wenzie kwenye maandamano.
Bodi ya madawa nchini MSD nao kwenye maandamano hayo.
TANAPA hawoooo..
TANROAD ujumbe wao ulikuwa 'Usijenge wala kufanya biashara au shughuli yoyote ndani ya hifadhi ya barabara'
TTCL nao wamo...
Katika risala yao wafanyakazi wa jiji la Mwanza wametamka wazi kuwa hawaoni jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali katika kupata ufumbuzi na kutatua matatizo ya msingi yaliyowahi kuwasilishwa Serikalini ili kuondoa kero kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
Licha ya Waajiri wengi nchini kugeuza kazi nyingi kuwa vibarua hali inayopelekea wafanyakazi wengi kukosa ajira za kudumu. Pia imetajwa kuwa kutowajibika kwa watendaji wa mifuko ya jamii kumewasaidia waajiri wengi wenye nia mbaya kuwasajiri uanachama wa mifuko hiyo na kuanza kuwakata michango bila kuwasilisha kwenye mamlaka husika na pindi wanapoachishwa kazi wafanyakazi hao hukuta hakuna michango yoyote iliyowasilishwa kwenye mfuko husika
Wafanyakazi wa majumbani nao walihusika kwenye sherehe hizi na wakawasilisha kero zao.
TAFAKARI: Mfanyakazi wa Tanzania anafanyakazi miaka 30 ndani ya utumishi bila kuwa na uwezo wa kununua hata godoro anakuja mgeni na kufanyakazi nchini, ndani ya mwaka mmoja anamiliki nyumba, gari na anamradi wake wa ziada... 

source www.gsengo.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA