ARGENTINA YATINGA FAINALI BAADA YA KUITOA UHOLANZI KWA PENATI 4-2

article-2686460-1F8654A700000578-278_634x481 (1) 

NDOTO za Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka huu katika ardhi ya majirani zao Brazil zimeendelea kuwepo baada ya kuipiga Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-2.
Mechi hii kali ya nusu fainali ya pili imekwenda mpaka dakika 120, lakini matokeo yalisimama 0-0.
Mlinda  mlango wa Agrgentina, Sergio Romero alikuwa shujaa baada ya kuokoa penati mbili za  Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
Waamerika kusini hao walifunga penati zao zote  nne na sasa watacheza fainali dhidi ya Ujerumani, siku ya jumapili katika dimba la Maracana.
Lionel Messi alibanwa na wachezaji wa Uholanzi na kushindwa kuleta madhara.
Naye Robin Van Persie alifichwa kabisa na alitolewa katika dakika za nyongeza.
article-2686460-1F86086B00000578-879_634x372  
Gonzalo Higuain alipoteza nafasi muhimu ya kufunga katika dakika za kawaida. 

Head-to-head: Ezequiel Garay and Robin van Persie collide in a painful mid-air collision
Kichwa kwa kichwa: Ezequiel Garay na Robin van Persie waligongana

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA