UFAFANUZI: HIKI WALICHOFANYIWA BRAZIL KAMWE HAKITASAHAURIKA

Michuano ya kombe la dunia jana usiku imechukua sura nyingine kabisa baada
ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya wenyeji Brazil dhidi ya
Ujerumani.
Kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Belo Horizonte – Ujerumani
wameweka historia ya mbili kubwa – kutinga fainali ya 8 ya kombe la
dunia – hii ni mara nyingi kuliko timu zote duniani, pili kuifunga
Brazil nyumbani kwao ikiwa ni mara ya kwanza kwa Brazil kupoteza mechi
ya ushindani kwenye ardhi yao tangu mwaka 1975.
Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Muller, Toni Kroos mawili, Sami
Khedira, Ander Schurrle nae akafunga mawili huku Oscar akiifungia Brazil
goli moja la kufutia machozi katika mechi iliyoishwa kwa ushindi wa
7-1.
Ujerumani sasa anamsubiri mshindi wa kati ya Argentina vs Uholanzi
hapo kesho ili kupata kujua mpinzani wake wa fainali itakayopigwa
jumapili hii.
Comments
Post a Comment