Mahakama yathibitisha kuwa Silinde ndiye Mbunge halali Mbozi Magharibi

Silinde
Mahakama
Kuu ya Rufaa Kanda ya Mbeya imeondoa shauri la kesi ya rufaa
iliyopelekwa na Dkt.Lucas Siame(CCM) kupinga hukumu iliyotolewa Julai
mosi, mwaka jana dhidi ya ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi
David Silinde (CHADEMA) hivyo kumfanya Silinde kuwa mbunge halali wa
jimbo hilo.Mamuzi huo ulitolewa leo na Majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo chini ya Mwenyekiti wao Jaji Januari Msofee ambao ni Jaji William Mandia na Jaji Mbarouk S. Mbarouk baada ya Wakili wa mlalamikaji Victor Mkumbe kuwakilisha ombi la kutaka kuondoa shauri hilo mahakamani hapo.
Akiwasilisha ombi hilo mbele ya mahakama hiyo ya rufaa wakili Mkumbe amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya mlalamikaji kuonyesha nia ya kutotaka kuendelea na kesi hiyoBaada ya maelezo hayo jaji Msofee amemhoji wakili wa mlalamikiwa Benjamini Mwakagamba kama angekuwa na la kusema baada ya kusikia ombi la mlalamikaji naye akakubaliana na ombi hilo lakini akiitaka mahakama kumwamuru mlalamikaji kumlipa gharama alizotumia.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Mandia amrsema kuwa mahakama ya rufaa imekubali ombi hilo na hivyo shauri hilo limeondolewa kwa mujibu wa kanuni ya 4(2)(a).
via blogu ya "Lyamba Lya Mfipa"
Comments
Post a Comment