TATIZO LA WEZI ENEO LA SAUT -MWANZA LAZIDI KUSHAMIRI
Mtu anayesadikiwa kuwa mwizi akichomwa moto leo majira ya asubuhi hapa chuoni saut.
picha ni kwa msaada wa mdau Monica makaluni.
Leo hii majira ya saa 3 asubuhi maeneo ya Vanessa katika hostel inahitwa Bismark mtu anayesadikiwa kuwa mwizi amekamatwa akiiba laptop, amepigwa mpaka kupoteza maisha.
Tatizo la ongezeko la wezi limekuwa likiongezeka kwa kasi ya ajabu kila kukicha katika maeneo mbalimbali yanayozunguka chuo cha Mt.Agustino (SAUT)-Mwanza ambayo yamekuwa yakikaliwa na wanafunzi wa chuo hiki (hostels). Wanafunzi wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa wakiofia hatima ya maisha yao yatakuwaje kwani sio mahali salama tena pa kuishi,kwa kuwa wezi hao wamekuwa wakibomoa milango yao nyakati za usiku na wengine wamekuwa wakikabwa mchana kweupee na kunyang'anywa vitu vyao kama simu,laptop n.k pindi wanapokuwa wanakuja kwenye lecture.
Kumekuwa na matukio mengi yakiripotiwa kuhusu wanafunzi kujeruiwa lakini bado hatua mathubuti za ukomeshaji wa tabia hii bado haujafanikiwa,kumekuwa kama vita kati ya wezi hao na wanafunzi....pindi unapojikuta umeingia mikononi mwao basi hawakuachi lazima wakujeruhi na pia kuchukua vitu vyako,kutoka na hali hiyo wiki mbili zilizopita mwizi mmoja alikama na kupigwa mpaka kupoteza maisha.
Blog hii inaomba chuo kiweze kuchukua hatua madhubuti kupambana na hali hii kama kuboresha ulinzi katika maeneo yote yanayokizunguka chuo na kuweza kushirikiana vizuri na jeshi la polisi kwani wanafunzi wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa hasa inapofika wakati wa usiku kwani hawajui kama kutaweza kucha bila tukio la wizi kutokea.

Comments
Post a Comment