MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA KIONGOZI WA CHADEMA-ARUSHA

DSCN0146Jeneza lenye mwili wa marehemu Msafiri Jonathan Mbwambo (38) likishushwa kwenye gari kwa maandalizi ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho katika viwanja vya Ngusero, Usa-River jana. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa chama, RPC wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, OCD wa Arumeru na wananchi wengine.
DSCN0169 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye (katikati) akifuatilia hotuba za wasemaji wa makundi ya jamii yaliyowakilishwa. Kutoka kushoto anaonekana kwa mbali Mh Vicent Nyerere (Musoma), Mh Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Mh Godbless Lema, Mh Cecilia (Viti Maalumu), Kamanda Andengenye, na OCD John wa Arumeru
DSCN0177Kamanda Andengenye akisalimia wananchi. Baadae aliahidi kuwa Jeshi lake litatoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa mtu atakaesaidia kupatikana kwa waliohusika na mauaji hayo na kwamba Polisi watahakikisha wanawasaka wahalifu hao kwa udi na uvumba hadi wapatikane.
DSCN0204Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari (CHADEMA) akizungumza kwa hisia kuhusiana na mauaji yanayowaandama viongozi wa chama chake
DSCN0231 Mbunge wa Musoma, Mh Vicent Nyerere akitoa heshima za mwisho. Mh Vicent ndie alieteuliwa kuwakilisha chama chake katika maziko yanayofanyika leo kijijini kwa Marehemu, Same-Kilimanjaro
DSCN0238Kuna walioshindwa kujizuia na kuishia kuangua kilio. Simanzi kubwa
DSCN0141  Msiba ulikuwa mchungu kwa kada nyingine za siasa pia, na si CHADEMA pekee
DSCN0246Kuna waliopandisha mori kama huyu mama. Hapa anaondolewa eneo la viwanja hivyo
DSCN0226 Aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akielekea kutoa heshima za mwisho akiwa ameambatana na mtoto wake. Nyuma yake ni Mbunge mpya Viti Maalumu, Mh Cecilia aliechukua nafasi ya marehemu Regia Mtema aliekufa kwa ajali ya gari mapema mwaka huu.
DSCN0162Watoto walioachwa na marehemu
DSCN0155Mke wa marehemu akifarijiwa na majirani zake
DSCN0334Baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana CHADEMA Mkoa wa Arusha wakijadiliana jambo ukiwa unasubiriwa msafara wa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Same uanze kuondoka 
 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA